volunteers
Wednesday, February 11, 2015
WATOTO WA MITAANI NA JINSI YA KUWASAIDIA
Ukatili dhidi ya watoto umeongeza idadi ya watoto
wanaoishi kwenye mazingira hatarishi licha ya
kuwepo juhudi za kupambana na tatizo hilo.
Watoto wanaoishi katika mazingira hayo, huathirika
kisaikolojia kutokana na kujiingiza katika vitendo
vya matumizi ya gundi na dawa za kulevya, huku
sehemu ya jamii katika ngazi ya familia na kuficha
tatizo badala ya kulipeleka kwenye vyombo vya
dola.
Wanafanya hivyo kwa maelezo kuwa wanaogopa
aibu, matokeo yake kuna ongezeko la watoto wa
mtaani, baadhi ambao bado wapo chini ya
matunzo ya wazazi wao, lakini wanajiingiza katika
tabia ya kuomba fedha na wanaonekana mitaani
katika miji mbali mbali nchini.
Ukatili unafanyika dhidi ya watoto kuanzia ngazi ya
familia na ndugu wa karibu kwa kumbaka au
kumlawiti mtoto anyeishi nao. Sheria ya mtoto
namba 21 ya mwaka 2009, inalenga kurekebisha
na kuimarisha sheria zote zihusuzo watoto,
kuainisha haki, kukuza na kulinda maslahi bora ya
watoto kwa mujibu wa sheria.
Kuna uwezekano wa kulitokomeza hili tatizo la
watoto wa mitaani, iwapo jamii itaamua kulichukua
na kulipa nafasi kubwa na mikakati madhubuti
katika kulitokomeza.
Kutokana na furusa zilizopo kwa nchi yetu,
kuwapatia hawa watoto shilingi mia au mia tano
sio njia sahihi ya kulitokomeza tatizo la watoto wa
miataani. Kuna uwezekano wa kuwapatia hawa
watoto elimu ili mwisho wa siku na wao pia
waweze kujitegemea badala ya kuwapatia mia tano
ambayo wataitumia kwa mlo mmoja na tatizo
linabaki palepale.
Pia kutokana na vipaji mbalimbali walivyonavyo
hawa watoto kuna uwezekano wa kuwaendeleza
kwa vipaji walivyonavyo ili kwa vipaji hivyo viweze
kuwasaidia maishani na waweze kuyaendesha
maisha yao wenyewe badala ya kushinda
barabarani wakiomba misaada.
Subscribe to:
Posts (Atom)